emblem

The United Republic of Tanzania

The National Museum of Tanzania (NMT)

BG IMAGE

Welcome to National Museum

Service Category

News

Miradi Shirikishi kwa Uhifadhi Endelevu


Na Mwandishi Wetu

Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga amewataka wadau mbalimbali katika maendeleo ya nchi kuanzisha miradi inayohusisha jamii kwa lengo la kulinda na kuhifadhi urithi wa asili na utamaduni wa Tanzania.

Dkt. Lwoga ameyaseema hayo alipokuwa alizindua Maonesho ya Wiki ya Urithi wa Bahari katika Ndaki ya Insia, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yenye Kaulimbiu ya Bahari ni Urithi Wetu:Tuithamini na Kuilinda kwa Maendeleo Jumuishi.

Akizungumza katika ghafla hiyo ambayo alialikwa kama Mgeni rasmi, Dkt Lwoga amesema kuwa miradi ya urithi wa asili na utamaduni inayohusisha wananchi au jamii ya eneo husika ni muhimu sana katika uhifadhi endelevu wa urithi huo.

Dkt. Lwoga aliipongeza Ndaki ya Insia ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kuanzisha miradi inayohusisha wananchi wa maeno husika katika kuhifadhi na kuendeleza urithi wa asili na utamaduni.

“Pongezi sana kwenu kwa kuanzisha miradi yenye kuhusisha jamii katika kuanzisha vikundi vya kutengeneza vyakula vya asili na kutengeneza ngalawa ambao ni uhifadhi wa ujenzi wa asili,” alisema Dkt Lwoga.

Kaimu Rasi wa Ndaki ya Insia, Dkt Aurelia Mallya alisema kuwa katika mradi huo wa Bahari Yetu, Urithi Wetu unaotekelezwa katika mwambao wa Pwani ya Bagamoyo na Kilwa unashirikisha jamii inayozunguka eneo la mradi.

Katika jamii hizo kumeanzishwa vikundi vya ujasiliamali vya kutengeneza vyakula vya asili na vya kutengneza ngalawa za asili kwa lengo la kuhifadhi urithi wa asili wa maeneo hayo.

“Tunafanya hivyo ili kulinda na kuhifadhi urithi wa asili unaopatikana katika mwambao wa Pwani” alisema Dkt Mallya.

Naye Mratibu wa Mradi wa Bahari Yetu Urith Wetu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt Elgidius Ichumbaki aliseema kuwa mradi huo unatekelezwa katika nchi ya Tanzania, Kenya na Msumbiji.

Lengo la Mradi huo ni kuhakikisha kuwa rasilimali zinazopatikana katika mwambao wa Pwani zinatumika kwa maendeleo endelevu kwa manufaa ya kizazi cha sasa cha baadayeA.

Maonesho ya Urithi wa Bahari yatadumu kwa muda wa siku saba kuanzia tarehe 30 Novemba mpaka tarehe 6 Desemba 2020 ambapo wananchi wote wanakaribishwa kufika ili kujifunza mambo mbalimbali yahusuo urithi wa bahari.Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Dkt. Noel Lwoga akipata maelezo kuhusu maonyesho hayo kutoka kwa Mratibu wa Mradi, Dkt. Elgidius Ichumbaki.