emblem

The United Republic of Tanzania

The National Museum of Tanzania (NMT)

BG IMAGE

Welcome to National Museum

Service Category

News

Prof. Saida Yahya Othman achangia Makumbusho ya Taifa Vitabu kuhusu Mwalimu Nyerere


Prof Saida Yahya Othman kwa niaba ya Prof Issa G. Shivji na Prof Ng'wanza Kamata ameikabidhi Makumbusho ya Taifa Vitabu vya Wasifu wa Hayati Baba wa Taifa Mwl Julias Nyerere (Biography ya Mwl Nyerere) ili vihifadhiwe kwa manufaa ya Kizazi cha sasa na kijacho.

Akipokea Vitabu hivyo Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga amempongeza Prof Saida kwa kuona umuhimu wa vitabu hivyo vihifadhiwe Makumbusho ya Taifa.

" Nijambo jema sana na la heshima kubwa alilolifanya Prof Saida maana licha ya urithi huu kuhifadhiwa pia utatumika katika kupata raarifa muhimu kuhusu Mwl Nyerere zitakazo wezesha uwanzishwaji wa Makumbusho ya Marais nchini" alisema Dkt Lwoga

Dkt Lwoga aliongeza kwa kutoa wito kwa wadau mbalimbali wenye vitu au taarifa muhimuzinazohusu urithi wa kiutamaduni na asilia kujitolea ili vihifadhiwe Makumbusho ya Taifa.