emblem

The United Republic of Tanzania

The National Museum of Tanzania (NMT)

BG IMAGE

Welcome to National Museum

Service Category

Events

MHE AMOS MAKALLA MGENI RASMI ONESHO LA SANAA NA WASANII (MUSEUM ARTS EXPLOSION)


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye maonesho ya Sanaa na wasanii (Museum Art Explosion) ya kila mwezi yanayo ratibiwa na Makumbusho ya Taifa kupitia kituo chake cha Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Bw Mawazo Ramadhani alipokuwa akikaguwa hatua za mwisho za uwekaji Maonesho hayo ambayo yanatarajiwa kuhudhuriwa wa watu mbalimbali wakiwemo viongozi na wataalamu wa Makumbusho kutoka nchi ya Malawi.