emblem

The United Republic of Tanzania

The National Museum of Tanzania (NMT)

BG IMAGE

Welcome to National Museum

Service Category

Events

Waziri Mkuu Mgeni Rasmi Kumbukizi ya Vita vya MajiMaji


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kasimu Majaliwa Majaliwa anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika kilele cha Maadhimisho ya Kumbukizi ya Vita vya MajiMaji na Tamasha la Utalii na Utamaduni linalotarajiwa kufanyika mjini Songea kuanzia tarehe 22 -27 Februari 2021.

Tamasha hili ambalo litazinduliwa rasmi na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe Dkt Damas Ndumbaro tarehe 25 Februari litaambatana shughuli mbalimbali ikiwemo, programu za kielimu na kijamii, kongamano la wadau kuhusu utalii, kutembelea vivutio vya utalii vilivyoko katika Mkoa wa Ruvuma na gwaride la heshima kuwaenzi mashujaa wa vita vya Majimaji