News
BALOZI O'NEILL AHIMIZA UPANDAJI MITI

Wanaichi wameshauriwa kupanda miti kwenye maeneo yao ili kurejeresha nchi katika hali ya kuwa na misitu ya kutosha itakayo wezesha kuwa na Mazingira salama kwa viumbe wote.
Hayo yamesemwa na Balozi wa Ireland nchini Mhe Mary O'Neill kwenye programu ya upandaji Miti iliyofanyika Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni, iliyo ratibiwa na Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Kijani Pamoja na Makumbusho ya Taifa nchini.
Mhe O'Neill licha ya kuupongeza uwongozi wa Kijani Pamoja na wa Makumbusho ya Taifa kwa jitihada zinazo onesha katikakupambana na uwaribifu wa Mazingira, amesema ofisi yake ipo tayari kuendeleza mashirikiano mazuri yaliyopo na Taasisi hizo hasa katika utunzaji wa mazingira.
Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Bw Achiles Bufure ameushukuru ubalozi huo wa Ireland nchini kwa kuungana na Taasisi hizo katika zoezi la upandaji miti kwenye viwanja vya Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam, na kuwa Makumbusho hiyo itaitunza miti iliyo pandwa ili iweze kuleta tija kwa jamii.
Akiizungumzia program hiyo ya upandaji miti, Kiongozi waTaasisi yaKijani Pamoja amesema zoezi Hilo la upandaji miti ni sehemu ya kusherekea siku ya Sayari Duniani inayo adhimishwa kila Machi 23 hivyo kwa mwaka huu wameona vyema kushirikiana na Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Mkubusho na Nyumba ya Utamaduni,Bw Achiles Bufure, akishiriki zoezi la upandaji miti katika Makumbusho hiyo.