emblem

The United Republic of Tanzania

The National Museum of Tanzania (NMT)

BG IMAGE

Welcome to National Museum

Service Category

News

MAADHIMISHO YA SIKU YA MALIKALE MIKINDANI YALETA FARAJA KWA WAKAZI WA MIKINDANI MTWARA


Na Sixmund J. Begashe

Watanzania wametakiwa kuthamini urithi wa Malekale ili kuendelea kuhifadhi urithi adhimu wa historia ya nchi yetu kwa faida ya kizazi kilichopo na kijacho.

Wito huo umetolewa na Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani Mhe Shadida Ndile kwenye uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Malikale yanayofanyika Mikindani Mtwara yenye lengo la kuelimisha umma juu ya uhifadhi endelevu wa Majengo ya kihistoria pamoja na kuhamasisha jamii kutembelea majengo hayo ili kujipatia elimu na burudani.

Mhe Ndile ameipongeza Makumbusho ya Taifa kwa hatua muhimu iliyoichukuwa ya kuendelea kukarabati majengo ya Kale ya Mji Mkongwe wa Mikindani na kuutangaza kupitia program zinazo shirikisha jamii kama vile matamasha na maonesho.

Mikindani ni mji unao vutia sana, una majengo ya kale, una bahari yenye fukwe nzuri sana, watu wa hapa ni wakarimu sana, tunapenda kuona watu wengi wanafika hapa ili kujionea urithi huu adhimu wa kihistoria na kujifunza wapi taifa letu lilikotoka na hapa tulipo” Aliongeza Mhe Ndile.

Akizungumzia Maadhimisho hayo, Mhifadhi wa Malikale Makumbusho ya Taifa ambaye ni Mratibu wa Maadhimisho hayo Bi Frida Kombe amesema wameamua kuwa na program nyingi elimishi pamoja na maonesho ya wadau wa Malikale ili kuipa jamii mawanda mapana ya uhafamuhu juu ya umuhimu wa urithi huo.

Wananchi wanaendelea kufurahia maadhimisho haya kupitia mafunzo ya namna ya kutunza urithi huu wa majengo ya kale, kucheza muziki, ngoma za asili za makabila ya hapa, maonesho ya wadau wa Malikale, michezo ya kufukuza kuku, kujibu maswali na kujipatia zawadi, kukuna nazi na muxhezo minginw ya asilo." alisema Bibi Kombe.

Bibi Kombe ameongeza kuwa tarehe 28 Agosti 2021 wanatarajia kupa Baraka za Mwenge wa Uhuru ambao utafika kwenye viwanja hivyo.

Mkazi wa Mikindani Bw Fakii Mohamedi alieleza kuwa wamefarijika sana kuona Mikindani yao Ikihuishwa tena hivyo wanatarajia kuona wageni wengi wakiwatembela jambo litakalo saidia kuinua uchumi wa wanamikindani na maeneo jirani.

Maadhimisho hayo ya Mwaka huu yenye kaulimbiu inayosema MALIKALE KWA UCHUMI ENDELEVU ambayo kilele chake ni tarehe 28 Agosti 2021 yatakuwa yakiadhimishwa kila mwaka kwenye maeneo mbalimbali yaliyobeba urithi wa historia ya MALIKALE.


Mhifadhi kiongozi wa Mji Mkongwe Mikindani Bw, Paul Ndahani (Kushoto) akimpatia maelezo Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani Mhe Shadida Ndile (wapili kulia) na ujumbe wake juu ya namna ya ukarabati wa majengo ya kale

Mhifadhi Mkuu wa Malikale Makumbusho ya Taifa Bw Revocatus Bugumba akitoa elimu ya uhifadhi wa Malikale kwa wananchi walio udhuria Maadhimisho ya wiki ya Malikale Mikindani Mtwara


Kikundi cha ngoma cha Mundu kikitoa burudani ya asili ya makabila ya Mtwara kwenye sherehe za wiki ya Maadhimisho ya Malikale Mikindani Mtwara

Wakazi wa Mikindani na maeneo mbalimbali ya Mtwara wakiwa katika sherehe za wiki ya Maadhimisho ya Malikale Mikindani Mtwara.