emblem

The United Republic of Tanzania

The National Museum of Tanzania (NMT)

BG IMAGE

Welcome to National Museum

Service Category

News

NGUVU YA MAKUMBUSHO KURITHISHA


Watanzania wametakiwa kushirikiana na Makumbusho ya Taifa la Tanzania katika uhifadhi wa urithi wa nchi kwa faida ya kizazi cha sasa na vijavyo.

Wito huo.umetolewa na Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni, Bw Achilea Bufure wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Makumbusho Duniani jijini Dar es Salaam.

Siku ya Makumbusho Dunia huandhimishwa kila mwaka tarehe 18 Mei na kaulimbiu ya mwaka 2022 ni Nguvu ya Makumbusho.

Bw. Bufure amesema makumbusho zina nguvu ya kuhifadhi na kurithisha urithi wa asili na utamaduni wa nchi hivyo Watanzania wanatakiwa kushirikiana na Makumbusho kwa uhifadhi emdelevu.

Nguvu nyingine ya Makumbusho ni katika kutoa elimu kwa jamii kupitia mikusanyo na tafiti mbalimbali zinazofanywa na wataalamu wa Makumbusho, amesema Bw Bufure.

Amesema Makumbuaho ya Taifa inafanya maboresho ya maonesho ili yawe ya kidigitali ili kuendana na maendeleo ya teknolojia duniani.

'Tunataka kuwa na maoneaho ya kisasa ambayo ni rahisi kufikika kwa wadau wa ndani na nje ya nchi amesema . Bw. Bufure.

Makumbusho ya Taifa imeadhimisha Siku ya Makumbusho Duniani kwa kuwaalika wanafunzi washule za sekondari za Benjamin Mkapa, Jitegemee, Osterbay nawadau wengine ambao waliweza kuonesha kazi mbalimbali za sanaa ikiwemo ngoma, maigizo, mashairi, na maoneaho ya mitindo mbalimbali ya mavazi.

Mwl. wa Shule ya sekondari ya Benjamin Mkapa Bw. Brighton Mbasha akizungumzankwa niaba ya walimu wenzake waliofika kwenye shughuli hiyo amesema Makumbusho ya Taifa ndio eneo pekee ambapo mwanafunzi anaweza kujifunza historia kwa vitendo, uzalendo, sanaa na tamaduni mbalimbali za nchi yetu.

' Nawashauri wazazi na waalimu kuwahimiza wanafunzi wao kutembelea makumbusho kwa sababu kuna mambo mengi ya kujifunza' amesema Mwl Mbasha.

Maelezo ya picha

Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni, Bw. Achiles Bufure akikata utepe kuashiria ufunguzi wa onesho maalumu kuhusu Siku ya Makumbusho Duniani iliyofanyika tarehe 18 Mei, 2022

Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Benjamini Mkapa ya Dar es Salaam wakicheza ngoma kama sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Makumbusho Duniani


Baadhi ya wanafunzi walioshiriki maadhimisho hayo Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni