emblem

The United Republic of Tanzania

The National Museum of Tanzania (NMT)

BG IMAGE

Welcome to National Museum

Service Category

News

Waziri Masanja azindua gari ya Maonesho yanayotembea (Mobile Exhibition Van).


Na Mwandishi Wetu, Songea

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja amezindua gari ya maonesho yanayotembea mjini Songea na kuitaka Makumbusho ya Taifa kuitumia katika kutangaza utalii wa makumbusho, malikale na utamaduni nchini.

Gari hilo lililonunuliwa na Makumbusho ya Taifa kwa lengo la kuwafikia wananchi wengi zaidi katika maeneo mbalimbali ikiwa sehemu ya Mpango Mkakati wa Taasisi wa kuwafikia wananchi kwa njia mbalimbali.

Aidha, Mapango wa Masoko wa Taasisi umeainisha njia mbilimbali za kutangaza makumbusho na malikale nchini ikiwemo maonesho, matangazo na programu za kielimu.

"Gari hili litumike katika kuutangaza utalii wa makumbusho, malikale na utamaduni nchini ili watu wengi zaidi wajifunze" amesema Mhe Masanja.

Gari hilo lilikuwa kuvutio kikubwa kwa wananchi wakatibwa maadhimisho ya Kumbukizi ya Vita vya MajiMaji katika maeneo mbalimbali ya mji wa Songea.

Naye Mkui wa Mkoa wa Ruvuma Col. Laban Elias Thomas amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za kununulia gari hilo lililo na huduma zote zinazohitajika kwa ajili ya maonesho ya kitaalam ya makumbusho na malikale.

"Gari hili ni muhimu katika kuwafikia wananchi waliombali na makumbusho na malikale"Amesema Col. Thomas.

Gari la Maonesho yanayotembea limenunuliwa kwa fedha zaMpango wa Ustawi wa Jamii na Kuthibiti Maambukizo ya UViKO 19.