emblem

The United Republic of Tanzania

The National Museum of Tanzania (NMT)

BG IMAGE

Welcome to National Museum

Service Category

News

WAZIRI MKUU MHE.KASSIM MAJALIWA ATOA WITO KWA WATU BINAFSI KUMILIKI MALIKALE


SONGEA MJINI: Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Kassim Majaliwa ametoa wito kwa Watanzania wenye nia kutaka kumiliki maeneo ya Malikale kuwa fursa hiyo ipo ya wao kumiliki na kuanzisha Makumbusho kama Sera ya Malikale ya mwaka 2008 ilivyofafanua.

Akifunga Tamasha la Kumbukizi ya miaka 114 ya Mashujaa wa Vita vya Majimaji na Utalii wa Utamaduni, Waziri Mkuu aliyewakilishwa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Innocent Bashungwa amesema maeneo ya Malikale ni vyanzo vya ajira hivyo Jamii iwekeze ili watu wengi waweze kujiajiri kupitia fursa hiyo.

Amesema maeneo ya Malikale ni ajira hivyo Jamii iigeukie fursa hiyo ili kuweza kuwavutia Watalii kutembelea maeneo hayo kwa ajili ya kujifunza na kuhanikiza uzalendo umoja na utaifa wetu.

Kuhusu Matamasha ya Malikale, Mhe.Bashungwa ameitaka Wizara ya Maliasili na Utalii kuendelea kuadhimisha kumbukizi hizo ili ziwe sehemu ya vivutio vya utalii nchini ambapo zitaongeza pato la Taifa.

Kwa upande wake, Mbunge wa Songea Mjini na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro amesema Manispaa ya Songea kwa kushirikiana na Makumbusho ya Taifa imeaanza kuitikia wito wa kuandaa klabu za historia na uzalendo kwa Wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari ili kuwawezesha Wanafunzi hao kujua historia ya Tanzania kama ambavyo Mhe.Rais John Pombe Magufuli alivyoagiza.

Tamasha hilo la kumi na mbili tangu lilipoanza kufanyika Mjini Songea kwa mwaka huu limefanyika kwa muda wa siku mbili kuanzia tarehe 25 likiwa na kaulimbiu isemayo " Maisha yao ni Fahari yetu " likidhihirisha bayana uzalendo waliokuwa nao Wazee wetu katika kupambana dhidi ya utawala dhalimu wa Wakoloni.