Maji maji Memorial War Museum
Makumbusho inayohifadhi na kuonesha Historia ya Vita vya Maji Maji vilivyotokea mwaka 1905 -1907, Makumbusho hii ipo Mkoani Ruvuma, kilomita moja kutoka katikati ya mji wa Songea
Mtaalam wa Makumbusho ya Maji Maji Mjini Songea, akimpatia maelezo mtalii wa ndani namna mji wa Songea ulivyokuwa miaka ya 1905
Kiti kilichotumiwa na Chifu wa Wayao Ambuje Mataka ni moja ya vitu vya thamani katika historia ya Vita vya Maji Maji inayo patikana kwenye Makumbusho ya Maji Maji Mjini Songea Mkoa wa Ruvuma.
Vazi la asili la kabila wangoni lililotokana na Magome ya miti ni sehemu ya onesho katika ukumbi wa historia ndani ya Makumbusho ya Vita vya Maji Maji, mjini Songea.
Watalii wakilitazama kaburi walikozikwa Mashujaa 66 wa Vita vya Maji Maji. Kaburi hili lipo Makumbusho ya Maji Maji mjini Songea Mkoani Ruvuma.
Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga (Kulia) pamoja na Mwanamziki maarufu nchini Bw. Nguza Viking (Babu Seya) na Mkewe Mhe. Desderie Haule ambaye ni ( Katibu Tawala Wilaya ya Muheza Tanga) wakitoka kuangalia Mnara wa Mashujaa uliopo ndani ya Makumbusho ya Maji Maji mjini Songea.