Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Makumbusho ya Taifa la Tanzania

Kijiji cha Makumbusho

Kijiji cha Makumbusho ni makumbusho ya wazi iliyoanzishwa mwaka 1967 kwa lengo la kukusanya, kutafiti na kuhifadhi utamaduni wa jamii za watanzania na hasa mitindo ya ujenzi wa nyumba za asili.

Makumbusho hii inaonyesha maisha halisi ya watanzania hadi kufikia miongo michache iliyopita kupitia nyumba na vifaa walivyotumia. Baadhi ya nyumba zilizojengwa hapa hazitumiwi tena wakati nyumba zingine hutumiwa na wanajamii wengi waishio sehemu za vijijini zikiwa zimeboreshwa au kuondolewa uasili wake.
Timu yetu yenye uzoefu itakusafirisha nchi nzima kwa wakati mfupi ukiwa sehemu moja. Ukiwa hapa jionee na furahia nyumba na vifaa vya asili, mboga na miti ya asili, maduka ya wajasiriamali yaliyosheheni bidhaa za mikono. Baada ya ziara yako mara ujihisipo umechoka na una njaa karibu katika mgahawa wetu na ujipatie chakula cha asili cha kabila upendaloama keti na uburudike na ngoma kutoka jamii za kitanzania.
Tembelea Kijiji cha Makumbusho na ujionee zaidi ya nyumba 30 za asili katika mitindo na maumbo ya:-

  • Tembe
  • Msonge
  • Banda