emblem

The United Republic of Tanzania

The National Museum of Tanzania (NMT)

BG IMAGE

Welcome to National Museum

Service Category

News

Bongozozo aikabidhi Makumbusho ya Taifa Sarafu ya Rupia iliyotengenezwa kwa Madini ya Tanzania


Balozi wa Utalii wa Tanzania, Bw Nick Reynolds maarufu kama Bongozozo akimkabidhi Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Bibi Adelaide Salema Sarafu ya Rupia 15 iliyotengenezwa hapa nchini mwaka 1916


Na Kitengo cha habari Makumbusho ya Taifa.

Balozi wa Utalii wa Tanzania, Bw Nick Reynolds maarufu kama Bongozozo ametoa wito kwa Watanzania kuwa na tabia ya kutoa vitu vyao vya thamani kwa Makumbusho ya Taifa kwa lengo ya kuhifadhi kwa ajili ya kizazi cha sasana vijavyo.

Bongozozo ameyasema hayo alipokuwa akikabidhi sarafu ya Rupia 15 iliyotengenezwa mwaka 1916 mjini Tabora na Mjerumani kwa Makumbusho ya Taifa ili iifadhiwe.

Makumbusho ndiyo mahali salama pa kuhifadhi vitu vya thamani kwa sababu ya taaluma ya uhifadhi waliyonayo wataalamu wa Makumbusho,” alisema Bongozozo.

Amesema ameamua kutoa sarafu hiyo kwa Makumbusho ya Taifa kwa sababu ya mapenzi yake nchi ya Tanzania.

Balozi wa Utalii wa Tanzania, Bw Nick Reynolds maarufu kama Bongozozo akijaza fumu maalumu ya kukabidhi Sarafu ya Rupia 15 iliyotengenezwa hapa nchini mwaka 1916 huku Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Bibi Adelaide Salema akishuhudia

Akizungumza katika hafla hiyo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Bibi Adelaide Salema amesema kuwa sarafu hiyo ni sehemu mhimu sana ya historia hususani katika kutambua mchango wa wahunzi na wasanifu madini waafrika/ watanzania (6) waliosailiwa na kufuzu mtihani wa umahili katika ufuaji madini na kuunganishwa na timu ya wataalamu kutoka katika mataifa mbalimbali kufanya kazi ya kufua na kutengeneza sarafu mjini tabora.

Amesema kuwa wasanifu kwa pamoja walikubalina kuwa miongoni mwa alama zilizowekwa katika Sarafu hiyo ni Mlima Kilimanjaro na mnyama Tembo, alama na isharaambavyo kwa mujibu wa taarifa na Kumbukumbu za historia zilitumika na wakoloni kama alama ya utajiri wa rasilimali na ufahari wa Taifa la Tanganyika the Gigantic wealth of Deutsch-Ostafrika.

“Tunamshukurua sana ndugu yetu na mdau wa historia ya Taifa letu Bw. Nick Reynolds(Bongozozo) kwa kuipatia Makumbusho ya Taifa sarafu hii” amesema Bibi Salema.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Bibi Adelaide Salema akimkabidhi Balozi wa Utalii wa Tanzania, Bw Nick Reynolds maarufu kama Bongozozo cheti cha kutambua mchango wake wa Sarafu ya Rupia 15 iliyotengenezwa hapa nchini mwaka 1916.

Mwaka 1916 Serikali ya kikoloni ilimleta nchini Tanganyika Prof. Schumacher kutoka Ujerumani, mtaalam msanifu wa madini ambaye aliongoza timu ya wataalamu wa kutengeneza na kuzalisha fedha za dhahabu katika karakana kuu ya reli Mjini Tabora.

Upekee wa historia ya sarafu hii ni kwamba katika timu ya wataalamu wasanifu wa madini iliyoongozwa na Prof. Schumacher, kati ya 16, miongoni mwao (2) ni wahindi wakazi, (1) Mzungu Mjerumani, (6) wahunzi waafrika, na (7) ni watu wenye asili ya kihindi kutoka Sri-lanka.

Sarafu hii ni miongoni mwa sarafu 16,198 pekee za Rupia 15 ambazo zilitengenzwa na wataalamu husika kuanza tarehe 15 April hadi Agosti, 1916 kabla ya Majeshi ya Waingereza na washirika wao wabelgiji hawajavamia nakuuteka mji wa Tabora tarehe 19 Septemba, 1916, hali ambayo ilipelekea kusitishwa kwa kazi hii ya Kihistoria.

Pichani ni Balozi wa Utalii wa Tanzania, Bw Nick Reynolds maarufu kama Bongozozo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Bibi Adelaide Salema, Kaimu Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Bw Philip Marigisu(mwisho kulia) pamoja na baadhi ya Maafisa wa Makumbusho ya Taifa.


Kwa mujibu wa taarifa na kumbukumbu za kihistoria dhahabu iliyotumika kutengenezea sarafu hii ilitoka katika mgodi wa dhahabu wa Senkenke umbali wa takribani Km. 25 magharibi mwa mji wa Tabora; toleo la sarafu hii lilikikadriwa kuwa na uzito wa gramu 7.168, ikiwa na mchanganyiko kwa wastani wa 75 % kuwa ni dhahabu na 15-20% kuwa ni madini ya fedha, na 5-10% ni shaba