Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Makumbusho ya Taifa la Tanzania

Makumbusho ya Mwl J.K Nyerere

Historia

Ujenzi wa Makumbusho ya Mwalimu Julius Nyerere ulianza mwaka 1987 chini ya wizara ya Elimu na Utamaduni na kukamilika mwaka 1999. Makumbusho haya yalifunguliwa rasmi tarehe 2 Julai 1999 na aliyekuwa Waziri Mkuu wakati huo Mhe. Frederick Tluway Sumaye. Mwalimu Nyerere pia alishiriki katika sherehe hizo.

Makumbusho ya  Mwalimu Julius Kambarage Nyerere yanahifadhi mikusanyo (collections) kuhusu historia ya Baba wa Taifa na mchango wake alioutoa kitaifa na kimataifa katika nyanja mbalimbali za maendeleo ya Taifa na harakati za  ukombozi wa bara la Africa.

Kwa ujumla makumbusho haya yana jukumu kubwa la kukusanya, kuhifadhi, kutafiti, kuelimisha na kuandaa maonesho yanayohusu historia ya maisha ya Baba wa Taifa na mchango wake kitaifa na kimataifa.

Miongoni mwa mikusanyo au vitu vilivyohifadhiwa na kuwekwa katika maonesho ya makumbusho haya ni pamoja na:

  • Zawadi alizopewa Mwl.J.K.Nyerere na Watanzania katika harakati za kudai Uhuru na baada ya uhuru
  • Zawadi alizopewa Mwl.J.K.Nyerere na Watanzania mwaka 1985 alipostaafu madaraka ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
  • Zawadi alizopewa Mwl.J.K.Nyerere na Watanzania baada ya vita ya Kagera (1979) kama alama ya ujasiri, ushujaa na uzalendo.
  • Zawadi alizopewa Mwl.J.K.Nyerere na watu na  serikali za  mataifa mbalimbali duniani ambazo Mwl.J.K.Nyerere alitembelea ama kutembelewa,
  • Baadhi ya vitu binafsi vya Mwl.J.K.Nyerere ambavyo  alivitumia katika maisha yake
  • Zawadi za kitaaluma alizopewa Mwl.J.K.Nyerere na Vyuo Vikuu mbalimbali duniani ( Shahada za heshima za udaktari wa Falsafa )

Makumbusho ya Mwl.J.K.Nyerere ni mahali pa kipekee ambapo watu wa rika zote wa ndani na nje ya nchi  hupata fursa ya kujifunza,kufurahia na kutafakari juu ya historia ya  maisha ya Mwl.J.K.Nyerere katika uongozi na maisha yake ya kawaida kama Mtanzania aliyejitoa mhanga katika kuleta uhuru wa Tanzania.

Hivyo basi taarifa zinazopatikana katika makumbusho haya ni urithi wa kipekee aliotuachia Baba wa Taifa  na ambao umehifadhiwa kwa faida ya kizazi cha sasa na vijavyo.

Shughuli zinazofanywa na Makumbusho ya Mwl. J. K.Nyerere

Kuendesha programu za elimu za kimakumbusho kwa:-

  1. Shule za msingi
  2. Shule za secondari
  3. Vyuo vya kati na juu
  4. Makundi maalumu ya watu wazima

Kuratibu matukio mbalimbali kituoni, ambayo ni:-

  • Mbio za Mwl. Nyerere Marathon
  • Kumbumbuku ya ya Kuzaliwa kwa MWL. Nyerere
  • Kumbukizi ya Kifo cha Mwl. Nyerere

Kupokea wanafunzi wa sekondari kwa ajili ya kufanya kazimiradi kulingana na mitaala yao shuleni

Kupokea wanafunzi wa vyuo vya kati na juu kwa ajili ya mazoezi kwa vitendo katika kutimiliza mahitaji ya masomo yao vyuoni

Kituo hufanya tafiti za kimakumbusho zinazohusiana na Mwl. Nyerere, pia kituo hupokea watafiti ambao hutafiti juu ya maisha na kazi za Mwl. Nyerere pamoja na tafiti za kimakumbusho

Kituo kunahifadhi mikusanyo mbalimbali yenye historia ya Mwl. Nyerere

Huduma zitolewazo na Makumbusho ya Mwl. Nyerere

Huduma hutolewa kwa wageni wanaotembelea makumbusho kwa ajili kujifunza maiasha na historia ya Mwl. Nyerere na Taifa la Tanzania kupitia maonesho yaliyopo kituoni.