MAKUMBUSHO YA TAIFA WAZINDUA RASMI VIFURUSHI VYA MSINU WA SIKUKUU.
MAKUMBUSHO YA TAIFA WAZINDUA RASMI VIFURUSHI VYA MSINU WA SIKUKUU.
Imewekwa: 09 Dec, 2024
Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa la Tanzania, Dkt. Noel Lwoga amezindua rasmi vifurushi vya msimu huu wa sikukuu kwa kuwaalika wananchi na wageni wote kwa ujumla kutumia fursa ya mapumziko ya sikukuu kwa kutembelea vituo vya Makumbusho na Malikale nchini.
Hafla hiyo imefanyika katika kituo cha Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Jijini Dar es Salaam.ambapo amewahimiza watanzania kujenga tabia ya kutembelea maeneo haya adhimu ya kihistoria na Malikale kwa kuwa kumeandaliwa programu maalum za kuwapa mafunzo na burudani wazazi na watoto wao kwa bei maalum.
Programu hizo zinajumuisha kuonja vyakula vya asili, michezo ya jadi, mashindano ya michezo mbalimbali kwa watoto na vijana na wanajamii kupata fursa ya kujikumbusha asili zao.