Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Makumbusho ya Taifa la Tanzania

Makumbusho ya Azimio la Arusha

Makumbusho ya Azimio la Arusha yanapatikana Mtaa wa Kaloleni jijini Arusha. Makumbusho haya yalifunguliwa rasmi mnamo tarehe 5 Februari, 1977 wakati wa kuadhimisha miaka 10 ya kutangazwa kwa Sera ya Ujamaa na Kujitegemea.

Makumbusho haya yanasadifu historia kubwa ya nchi yetu  Kijamii, kiuchumi na kisiasa kabla ya utawala wa wakoloni, wakati wa utawala wa wajerumani na waingereza, harakati za kudai uhuru, muungano wa Tanganyika na Zanzibar, sera za Azimio la Arusha, mchango wa Tanzania katika ukombozi wa Bara la Afrika na maendeleo ya hivi karibuni.

 

Baba wa Taifa Mwl. J. K. Nyerere akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Makumbusho ya Azimio la Arusha tarehe 5 Februari 1977

Mawasiliano

Makumbusho ya Azimio la Arusha

P.O BOX 7423 Arusha,

Tanzania

Mobile +255 678 853477

Email: adm@nmt.go.tz