Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Makumbusho ya Taifa la Tanzania

Makumbusho ya Vita ya Majimaji

Majimaji Memorial Museum In Songea, RUVUMA

A Destination to Honour Heroes

Makumbusho ya Kumbukumbu ya vita vya Majimaji ndiyo makumbusho pekee nchini Tanzania ambayo yanahifadhi na kulinda historia ya vita hiyo na baadhi ya silaha na zana halisi za asili zilizotumika wakati wa Vita vya Majimaji ikiwemo ngao (vikopa,) shoka za vita (vinjenje), vilabu (vibonga), na mikuki (migoha). Pia, baadhi ya picha halisi za wapiganaji walionyongwa tarehe 27 Februari 1906 na maeneo ya historia kama kaburi la halaiki, kaburi la chifu Songea na Eneo lililotumika kunyongea wapiganaji wa vita vya Majimaji mjini Songea.

Eneo la kunyongewa (Songea )

Eneo hili linafahamika zaidi kama manyongeo ni eneo maarufu na la kihistoria unapofika ndani ya mji wa Songea katika eneo hili ndio mahali palipotumika tangu enzi za ukoloni na ndio eneo ambalo lililotumika kunyongea mashujaa 66 waliopigana kipindi cha vita vya  Majimaji, eneo hili la manyongeo limekuwa eneo la kumbukumbu zaidi kwa jamii ya watu wa Songea na mkoa wa Ruvuma kwa ujumla hasa kwa wahanga wa vita vya Majimaji ndio sehemu ambayo wananchi walikusanyika na kushuhudia mababu, baba, wajomba na ndugu zao wengine wakinyongwa na Mjerumani mpaka kifo.

Kaburi la Halaiki

Moja ya kivutio muhimu na cha kihistoria kinachopatikana katika makumbusho ya kumbukumbu ya vita vya Majimaji ni kaburi la halaiki, kaburi hili ndio kaburi pekee linalopatikana nchini Tanzania na ndio kaburi pekee lililozika idadi kubwa ya watu kwa pamoja katika kaburi la halaiki ndio eneo ambalo walizikwa wapiganaji wa vita vya Majimaji kwa upande wa Tanganyika, na ndio kaburi pekee ambalo liliandaliwa na watu ambao wamezikwa ndani ya kaburi hilo, Mashujaa wa Tanganyika waliopigana katika vita vya Majimaji dhidi ya mkoloni (Mjerumani) walipokamatwa na kuwekwa gerezani walipewa adhabu kubwa ya kuchimba shimo lenye upana mkubwa na kina kirefu bila wao wenyewe kujua shimo hilo litatumikaje mara baada ya kumaliza kazi hiyo walirudishwa gerezani na ilipofika tarehe 27/02/1906. Mashujaa 66 walinyongwa na kuzikwa pamoja katika kaburi ambalo waliandaa wenyewe, kaburi hili linapatikana katika mtaa wa Mashujaa kata ya Mahenge wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma ndani ya viwanja vya Makumbusho ya Majimaji.

Kaburi la Nduna Songea Mbano.

Nduna Songea mbano ni moja ya mpiganaji wa vita vya Majimaji katika kundi la wapiganaji wa kingoni dhidi ya Wajerumani na ndiye aliyekuwa kiongozi mkuu wa vita vya Majimaji kwa upande wa wangoni Nduna Songea Mbano kwa cheo chake ndiye aliyekuwa msaidizi mkuu (Principal Nduna) wa chifu mkuu (Inkosi Ya Ma Inkonsi) na ndiye aliyepewa jukumu kubwa la kuongoza vita vya Majimaji katika eneo zima la Songea na kuongoza wapiganaji wengine wote kupigana dhidi ya Wajerumani, Nduna Songea Mbano alikuwa na mbinu nyingi za kivita na za kimila mpaka kupelekea Wajerumani kuwa na hofu kubwa dhidi yake na ndiye mpiganaji pekee wa vita ya Majimaji kutoka Tanganyika aliyeshindikana kuuwawa na Wajerumani na baadae kuamuru kuuliwa baada ya kuona hawezi kuendelea kuishi katika dunia ya manyanyaso namna hii, na baadae jina la mji wa Songea kupewa jina lake kutokana na umaarufu wake na mchango wake mkubwa kipindi chote cha vita, Kaburi la Nduna Songea Mbano linapatikana katika mtaa wa Mashujaa kata ya Mahenge wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma ndani ya viwanja vya Makumbusho ya Majimaji.

Mapango ya mlima chandamali

Mapango ya mlima chandamali ni moja ya sehemu iliyotumiwa kimkakati na kiongozi wa vita vya Majimaji Nduna Songea Mbano eneo hilo linapatikana nje kidogo kutoka katika viwanja vya Makumbusho ya Majimaji eneo la mlima chandamali ndio eneo yanapopatikana mapango ambayo yalitumika kipindi xha vita ya Majimaji kama sehemu ya maficho kwa chifu Songea Mbano pia juu ya mapango hayo ndipo alipokuwa anatumia kukaa na kuangalia maadui zake wakiwa katika umbali mrefu, katika mapango ya mlima chandamali shughuli mbalimbali za mila na desturi zilikuwa zikifanyika nab ado zinaendelea kufanyika mpaka sasa na ndio eneo pekee lenye sifa ya kuwepo kwa nyoka mkubwa wa kimila tangu kipindi cha vita vya Majimaji mpaka sasa, katika eneo hili pia ni moja ya sehemu ambazo mjerumani alishindwa kuingia na kukamata wapiganaji wa vita vya Majimaji.

What to do

Education activities, Research activities, Historical and Political Tours, Cultural and Traditional activities, Dark tourism and Filming.

Facilities

Shopping centre,

Curio shop,

Garden space and Restaurant.

Events and Dates

Majimaji Festival 23 - 27 February every year

Ge­tting There

 The Museum is located at Mashujaa Street along Mahenge Road, Songea Municipality in Ruvuma.

Contact:

Majimaji Memorial Museum

P.O BOX 1249 Songea,

 Tanzania

Mobile: +255 786 472700

Email: majimaji@nmt.go.tz