emblem

The United Republic of Tanzania

The National Museum of Tanzania (NMT)

BG IMAGE

Welcome to National Museum

Service Category

News

NAMNA ARDHI OEVU INAVYOWANUFAISHA WANAWAKE TANZANIA


Pichani kushoto ni Mhifadhi Mwandamizi wa Baolojia wa Makumbusho ya Taifa, Bibi Agnes Robert akiwafundisha wanafunzi mbali mbali wa Jijini Dar es Salaam, faida ya uhifadhi wa mazingira kwa ardhi oevu


Pichani kulia ni Mhifadhi Mwandamizi wa Baolojia wa Makumbusho ya Taifa, Bibi Adelaide Salema akiwafundisha wanafunzi mbali mbali wa Jijini Dar es Salaam, namna ya kufanya utafiti wa mimea, viumbe vya majini na nchikavu ili kulinda Ardhi Oevu.


Pichani kushoto ni Afisa Elimu wa Makumbusho ya Taifa, Bibi Wilhelmina Joseph akionesha moja ya kielelezo cha kufundishia kilichotengeneza na wanafunzi wa Shule ya Mshingi Minazini Dar es Salaam.Mmoja wa wanafunzi walioudhuria program elimu kuhusu uhifadhi wa ardhi oevu, akipanda mmea kando kando ya kijito cha maji kilichopo Kijiji cha Makumbusho jijini Dar es SalaamMmoja wa watalii akifurahia Madhari tulivu katika msitu wa asili uliopo kijiji cha Makumbusho Jijini Dar es Salaam.


Na Mwandishi Wetu

Makumbusho ya Taifa kupitia kituo chake cha Kijiji cha Makumbusho kilichopo Dar es Salaam kimeandaa programu maalumu ya kutoa elimu kuhusu umuhimu wa ardhi oevu kwa wanafunzi na wananchi kwa ujumla.

Katika programu hiyo iliyoandaliwa kwa kushirikiana na wadau inayojulikana kama Makumbusho na Sayansi, wanafunzi kutoka shule za misingi, sekondari na vyuo walipewa elimu kuhusu utunzania wa mazingira ya ardhi oevu kwa faida ya sasa na vizazi vijavyo.

Mratibu wa Programu hiyo, Bibi Agness Robert amesema kuwa programu hiyo inalenga katika kuwafundisha wanafunzi na wananchi kwa ujumla umuhimu wa kutunza mazingira, hususan ardhi oevu ambayo inasaidi katika kutunza viumbe hai na mimea.

Kaulimbiu ya Makumbusho na Sayansi mwaka huu ni “Mwanamke na ikolojia ya ardhi oevu” kwa maana kwamba mwanamke ni kielelezo muhimu katika utunzaji wa mazingira kutokana na shughuli anazozifanya. Hivyo tumeona ni muhimu kutoa elimu kwa manamke juu ya uhifadhi wa ardhi oevu kwa manufaa ya familia na jamii nzima inayomzunguka.

“Mwanamke amekuwa akipambana na mazingira kuhakikisha familia inapata mahitaji muhimu kama chakula, maji, na makazi safi na salama kwa familia yake” amesema Bibi Agness.

Mhifadhi Mwandamizi wa Biolojia, Bibi Adelaide Sallema amesema kuwa ardhi oevu ina aina mbalimbali za viumbe hai ikiwemo mimea ya asili, wadudu, wanyama wado wadogo, ndege na samaki.

Amesema ardhi oevu inafaida nyingi ikiwemo kuhifadhi mazingira, kuongeza aina vya viumbe hai (hutumika kama makazi ya wadudu, wanyama na mimea), kukuza utalii, kutoa elimu na utafiti wa kisayansi.

Bibi Sallema ametoa wito kwa wananchi kutunza mazingira na ardhi oevu ili kuepusha nchi na jangwa ambapo huwezi kuzalisha wala viumbe hawawezi kuishi.

Naye Mhifadhi Mila wa Kijiji cha Makumbusho Bibi Flora Vicent amesema kuwa Kijiji cha Makumbusho kina aina tofauti za mimea ya asili ambayo imepandwa kuzunguka nyumba za asili kutoka katika jamii mbalimbali za Tanzania.

Kijiji cha Makumbusho pia kina msitu wa ekari tano ambamo kuna njia za asili, wanyama, wadogo wadogo, ndege, wadudu, samaki na wadudu wa ardhi oevu ambavyo vimekuwa kivutio kikubwa kwa watalii wa ndani na nje ya nchi.

Programu hiyo iliandaliwa kwa kushirikiana na wadau wa Shirika la Jane Goodall- Roots and Shoots.