emblem

The United Republic of Tanzania

The National Museum of Tanzania (NMT)

BG IMAGE

Welcome to National Museum

Service Category

News

​ONGEZENI UBUNIFU WA MIRADI: WAZIRI CHANA


Na Mwandishi Wetu

Waziri wa Maliasili na Utalii. Mhe. Balozi. Dkt. Pindi Chana ameitaka Makumbusho ya Taifa kuongeza ubunifu wa miradi itakoyoweza kuongeza idadi ya watalii na kuongeza kipato kwa Taifa.

Mhe. Dkt. Pindi Chana ameyasema haya mwishoni mwa wiki (14 Mei 2022) alipotembelea Makumbusho ya Taifa, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupata ufahamu wa majukumu ya Taasisi hiyo.

Amesema kuwa kuna haja ya kubuni miradi mingi zaidi ya kuongeza watalii na kuongeza mapato kwa Taifa ili kuendana na malengo ya nchi ya kuongeza watalii kufikia billion tano.

Mhe. Dkt. Pindi Chana amesema kuwa sekta za Makumbusho na Malikale zina faida maradufu kwa jamii kwa ajili ya kuhifadhi histroria, utamaduni, uzalendo na kuongeza mapato kwa Taifa.

“Ninawapongeza kwa kazi kubwa na nzuri mnayoifanya ya kuhifadhi urithi wa asili na utamaduni wa nchi yetu,” alisema Mhe. Dkt. Chana.

Pamoja na kuipongeza Makumbusho ya Taifa kwa kazi nzuri ya uhifadhi wa Makumbusho na Malikale amesema kuna haja ya kubuni miradi mingi zaidi ya kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea vituo makumbusho na malikale hivyo kuongeza mapato kwa Taifa.

Waziri wa Maliasili na Utalii amempongeza Mhe. Raiswa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassani kwa ajili ya kutengeneza filamu ya Royal Tour ambayo inalenga katika kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea Tanzania, wawekezaji katika maeneo mbalimbali na kuongeza mapato ya nchi.

“Sisi kama Wizara ya Maliasili a Utalii tumependelewa sana kupitia filamu hii hivyo tunatakiwa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa tunaweaka mazingira mazuri kwa ajili ya watalii na wawekezaji watakao kuja Tanzania,” amesema Mhe. Waziri.

Amesema Mhe Raisi ametuonyesha njia ya kupita hivyo, Makumbusho ya Taifa inatakiwa kuangalia ni kwa namna gani inatumia fursa ya Royal Tour kwa maendeleo endelevu ya sekta ya makumbusho na malikale.

Awali, Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho, Dkt Noel Lwoga alisema kuwa Makumbusho ya Taifa imeandaa Mpango Mkakati wa 21/22 -2025/26 ambao umeanisha maboresho mbalimbali ya makumbusho na malikale.

Maelezo ya picha

Waziri wa Maliasili na utalii alipotembelea Makumbusho ya Taifa

Mhe Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Pindi Chana wa tatu kushoto na Mkurugenzi Mkuu, Dkt Noel Lwoga wa Makumbusho kulia kwake wakiwa katika eneo la baraza la Wakinga, Kijiji cha Makumbusho

Mhe. Waziri, Balozi. Dkt. Pindi Chana katikati akitembea ndani ya msitu wa Kijiji cha Makumbusho. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Dkt Noel Lwoga na kushoto kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa Makumbusho, Bw. Mawazo Jamvi


Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt Pindi Chana akiwa amebeba ungo aliopewa alipotembelea Kijiji cha Makumbusho

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Pindi Chana akiwa ameshikilia Mwenge wa kwanza uliotunzwa Makumbusho ya Taifa

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Pindi Chana akisoma hati ya uhuru iliyosainiwa na Malikia wa Uingereza ambayo Tanzania ilipewa wakati wa uhuru

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Pindi Chana akiwa ameshikiria vibuyu vya muungano alipoyembelea Makumbusho ya TaifaMkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Dkt. Noel Lwoga akimkabidhi zawadi ya kikombe chenye nembo ya makumbusho Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Pindi Chana