emblem

The United Republic of Tanzania

The National Museum of Tanzania (NMT)

BG IMAGE

Welcome to National Museum

Service Category

News

Balozi wa Marekani afanya mazungumzo na Waziri Kigwangala na kutembelea Makumbusho ya Taifa


Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Hamisi Kigwangala akifanya mazungumzo na Balozi wa Marekani nchini, Mhe Donald J. Wright katika viwanja vya Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.


Balozi wa Marekani nchini, Mhe Donald J. Wright akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga kwenye onesho lijulikanalo kama ‘MATUMAINI BAADA YA HUZUNI” lenye mabaki yaliyotoka kwenye Ubalozi wa Marekani uliolipuliwa na magaiditarehe 7 Agosti 1998 Jijini Dar es Salaam.


Balozi wa Marekani nchini, Mhe Donald J. Wright akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga kuhusu Magari ya kihistoria yaliyotumiwa na Hayati Baba wa Taifa Mwl Julias K. Nyerere.


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt Hamisi Kigwangala amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Mhe Donald J. Wright na kuzungumzia mashirikiano katika kutangaza vivutio vya utalii kupitia Teknolojia za kisasa na watu maarufu wa nchini Marekani, kuimarisha ulinzi kwenye maliaasili zetu pamoja na kuvutia wawekezaji katika sekta ya utalii nchini.

Dkt Kigwangala amesema, Taifa la Marekani ni mdau muhimu katika sekta ya Utalii nchini kwani yapo makampuni makubwa kutoka nchini humo yaliyowekeza katika nyanja mbali mbali ikiwemo ya malazi kwa watalii wanaotembelea vivutio vilivyopo katikahifadhi za Taifa.

’Tungependa watusaidie katika matangazo kupitia teknolojia ya kisasa, Filamu, Watu maarufu kama wanamichezo, waigizaji, pia kupitia makampuni makubwa hususani yanayo jishughulisha na michezo lakini pia Ulinzi wa Maliasili zetu pia kuvutia zaidi wawekezaji katika sekta hii ya Utalii hapa nchini” Aliongeza Dkt Kigwangala

Baada ya mazungumzo na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Kigwangala, Balozi huyo wa Marekani hapa nchini alipata nafasi ya kuitembelea Makumbusho ya Taifa na kujionea onesho lijulikanalo kama ‘MATUMAINI BAADA YA HUZUNI” lenye mabaki yaliyotoka kwenye Ubalozi wa Marekani uliolipuliwa na magaiditarehe 7 Agosti 1998 Jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia ziara hiyo ya Balozi wa Mrekani, Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga amesema ni kitendo kinachoonesha kuwa Tanzania ni salama navituo vya Makumbusho ya Taifa kama sehemu ya vivutio vya utalii ni Sehemu salama kiafya na kiulinzikwa wageni wote ambao ni watalii wa ndani na wale wa kutoka nje ya nchi.

“Ziara hii inaonesha dunia kwamba Tanzania ni salama, na imedhibiti vyema masuala ya ugaidi na janga la corona” anasema anasema Dkt Lwoga.

Dkt. Lwoga amesema kuwa vivutio vya utalii Tanzania ni salama kutembelewa na wageni wa ndani na nje ya nchi, hivyo watu wote waendelea kutembelea Makumbusho zetu zilizopo Dar es Salaam, Arusha, Butiama, Songea, pamoja na vituo vya malikale vilivyopo sehemu mbalimali nchini ikiwemo Mkindani Mtwara.