emblem

The United Republic of Tanzania

The National Museum of Tanzania (NMT)

BG IMAGE

Welcome to National Museum

Service Category

News

Makumbusho kuboresho ukusanyaji mapato


Na Mwandishi Wetu

Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Dkt. Noel Lwoga ameweka wazi vipaumbele vya taasisi hiyo kwa mwaka 2020/2021 kuwa ni kuboresha mapato ya taasisi kwa kubuni vyanzo mbalimbali vya mapato yatakayowezesha kutekeleza majukumu ya msingi ya taasisi hiyo.

Dkt. Lwoga ameyasema hayo katika kikao na wafanyakazi wote kilichofanyika katika kituo cha Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni jijini Dar es Salaam.

Amesema taasisi yake itaimarisha ukusanyaji wa mapato na utekelezaji wa shughuli za msingi za taasisi hiyo ambazo ni pamoja na kufanya utafiti,uhifadhi, na kutoa elimu kwa jamii kuhusu urithi wa asili wa Taifa la Tanzania.

“Lengo letu ni kuboresha utekelezaji wa majukumu ya taasisi kwa kuhakikisha kuwa urithi wa asili na utamaduni wa Taifa letu unahifadhiwa kwa gharama zozote,” anasema Dkt. Lwoga.

Amebainisha kuwa maandiko mbalimbali tayari yameandaliwa yatakayowezesha Shirika hilo kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi zaidi na kuboresha ukusanyaji na utunzaji wa mikusanyo.

Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa amewataka watumishi wa taasisi hiyo kufanyakazi kwa bidii, juhudi na maarifa ili kuweza kupata matokeo chanya.

“Kila mmoja wetu atumie ujuzi alio nao katika kuleta tija katika sekta ya utalii wa malikale na uzalendo kwa nchi yetu,” anasema Dkt. Lwoga.

Katika mkutano huo watumishi walimpongeza Dkt. Lwoga kwa hatua mbalimbali za maboresho ya taasisi anazozifanya na waliweza kubainisha changamoto wanazopambambana nazo katika utekelezaji wa majukumu yao.

Mwisho