Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Makumbusho ya Taifa la Tanzania

MAKUMBUSHO KUSHIRIKIANA NA UDART KUENDELEZA UTALII WA MALIKALE DAR

Imewekwa: 11 Jan, 2024
MAKUMBUSHO KUSHIRIKIANA NA UDART KUENDELEZA UTALII WA MALIKALE DAR

Makumbusho ya Taifa la Tanzania imeingia makubaliano na Wakala wa Mabasi yaendayo kasi UDART kuendeleza utalii wa malikale jijini Dar es Salaam, ikiwemo kutumia mabasi yake kutoa elimu kwa umma, kutangaza na kufanya ziara za kitalii kwenye urithi wa asili na utamaduni wa Tanzania unaohifadhiwa katika vituo vya makumbusho na malikale.

Makubaliano hayo yamefikiwa leo tarehe 20 Desemba 2023 katika kikao baina ya Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa la Tanzania, Dkt.Noel Lwoga na Afisa Mtendaji Mkuu wa UDART, Bw Gilliard Ngewe pamoja na Wataalamu kutoka Makumbusho ya Taifa la Tanzania na Wakala wa Mabasi yaendayo haraka kilichofanyika katika kituo cha Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni jijini Dar es salaam.

Aidha, katika msimu wa sikukuu mashirikiano hayo yataanza kwa mabasi ya UDART kutangaza vivutio vya Makumbusho ya Taifa la Tanzania ili jamii ifahamu programu za utalii na kutembelea Makumbusho katika msimu huu wa likizo.