Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Makumbusho ya Taifa la Tanzania

Makumbusho ya Taifa la Tanzania Yaanza Kutumia Lugha ya Alama Kukuza Ujumuishaji na Upatikanaji wa Taarifa

Imewekwa: 22 Apr, 2026
Makumbusho ya Taifa la Tanzania Yaanza Kutumia Lugha ya Alama Kukuza Ujumuishaji na Upatikanaji wa Taarifa

Makumbusho ya Taifa la Tanzania imeanza kutumia wataalam wa lugha za alama ili kuhakikisha ujumbe unawafikia watu wenye mahitaji maalum, hususan wenye ulemavu wa kusikia. Hatua hii inalenga kukuza ushirikishwaji na upatikanaji wa huduma za kielimu na kitamaduni kwa makundi yote ya jamii, kwa kuwezesha tafsiri ya maelezo ya maonesho na shughuli mbalimbali zinazofanyika ndani ya makumbusho.

Kupitia mpango huu, wageni wanaotumia lugha ya alama sasa wanaweza kufuatilia historia, urithi wa taifa, na tafiti mbalimbali kwa uelewa zaidi na usawa. Makumbusho imeonesha dhamira ya dhati ya kuifanya huduma yake iwe jumuishi, ikizingatia haki ya kila mtu kupata taarifa bila vikwazo.