emblem

The United Republic of Tanzania

The National Museum of Tanzania (NMT)

BG IMAGE

Welcome to National Museum

Service Category

News

Tanzania ipo tayari kupokea Watalii kutoka China


Waziri wa Maliasili na Utalii nchini Dkt Hamisi Kigwangala amefanya Mazungumzo na Mhe Balozi wa China nchini Mhe Wang Ke katika Viwanja vya Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es salaam.

Katika Mazungumzo hayo Mhe Kigwangala amemueleza Balozi Wang Ke kuhusu hatua mbali mbali zinacho chukuliwa na Serikali katika kukabiliana na janga la Korona na kwamba Tanzania ni Salama hivyo Wizara inaendelea kupokea watalii kutoka Mataifa mbali mbali Duniani.

Nae Balozi Wang Ke ameipongeza Serikali ya Tanzania chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa namna ilivyo weza kudhibiti Korona.

"Serikali ya Tanzania Imefanya kazi nzuri sana, kunawatu wetu wanaoishi hapa Tanzania waliugua Koroni lakini hadi sasa wote wamepona. Tunafatilia kwa karibu sana mahospitalini hakika tunaendelea kujifunza kutoka Tanzania jinsi mlivyo idhibiti Korona bila kuwafungia watu (quarantine)" alisema Balozi Wang Ke.

Mhe Waziri Kigwangala amemuhakikishia Balozi Wang Ke kuwa Wizara yake imeweka mazingira salama kwa watalii wote watakao ingia na kutoka nchini.