Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Makumbusho ya Taifa la Tanzania

WATANZANIA WAHAMASISHWA KUFUNGUA MAKUMBUSHO BINAFSI

Imewekwa: 27 Jan, 2024
WATANZANIA WAHAMASISHWA KUFUNGUA MAKUMBUSHO BINAFSI

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki amewataka Watanzania kufungua Makumbusho zao binafsi kwa mujibu wa Sheria ili historia na kumbukumbu muhimu ziweze kubakia kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Mhe. Kairuki ametoa kauli hiyo  leo tarehe 26/01/2024 akifungua onesho kuhusu Mahusiano baina ya Tanzania na India katika kituo cha Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni jijini Dar es Salaam shughuli iliyoendana sambamba na Maadhimisho ya Miaka 75 ya Uhuru wa Taifa la India.

"Ziko taratibu wakija hapa Makumbusho wataelekezwa, kuna ambao watataka kuanzisha makumbusho ya ukoo, makumbusho za taasisi, tunawakaribisha nyote mpate miongozo ili muweze kufanikisha ndoto na azma yenu"

Kwa upande wake Naibu balozi wa India nchini Tanzania, Mhe. Manoj Varma ameomba Taasisi ya Makumbusho ya Taifa kulifanya onesho hilo kuwa la kudumu kwa kuzingatia mahusiano ya muda mrefu ya mataifa hayo tangu Karne ya 19 kwenye nyanja za kijamii, kiuchumi na kisiasa.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa la Tanzania, Dkt.Noel Lwoga amesema ufunguzi wa onesho hili ni mwanzo wa kuanzishwa kwa Makumbusho binafsi ya Taifa la India itakayokua hapa nchini ili kuendelea kurithisha historia ya mahusiano baina ya mataifa haya mawili kwa vizazi vijavyo.