Dr. Rashid Mfaume Kawawa Museum Exhibition
Makumbusho ya Kumbukumbu ya Dkt. Rashid Mfaume Kawawa ni Tawi la Makumbusho ya Taifa la Tanzania. Makumbusho haya yalifunguliwa rasmi 27 /02/2017. Makumbusho ya Dkt. Rashid Mfaume Kawawa inapatikana Mtaa wa Kawawa, eneo la Bombambili, Wilaya ya Songea, Mkoa wa Ruvuma. Makumbusho haya yanahifadhi historia kuhusu maisha binafsi, maisha ya kisiasa na vitu mbali mbali alivyotumia aliyekuwa Kiongozi mwenye utumishi adhimu na uliotukuka Dkt. Rashid Mfaume Kawawa “Simba wa Vita” wakati akiwa Waziri Mkuu wa Pili na Makamu wa Rais na Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (awali Tanganyika). Maisha yake yanaonekana katika vitu alivyotumia enzi za uhai wake.